Nyanda za Juu za Bie
(Elekezwa kutoka Nyanda za juu za Bie)
Nyanda za Juu za Bie ziko kwenye kitovu cha nchi Angola. Zinapanda hadi ya kuwa na kimo cha 2,619 m juu ya UB.
Kutokana na kiasi kikubwa cha mvua kinachopatikana hapa eneo ni chanzo cha mito mingi muhimu ya Afrika ya Kusini na Afrika ya Kati.
Mito muhimu inayoanza Nyanda za Juu za Bie
hariri- Kwanza (Cuanza) - inaelekea kaskazini - magharibi na kuishia Atlantiki
- Kasai inaelekea kaskazini na kuishia mto Kongo
- Kwango inaelekea kaskazini na kuishia kwenye mto Kasai ndani ya Kongo.
- Kwando (Cuando) - inaelekea kusini-mashariki na kuishia Zambezi
- Kubango-Okavango - inaelekea kusini halafu kusini-mashariki na kuishia Delta ya Okavango kwenye Kalahari
- Kunene (Cunene) - inaelekea kusini-magharibi na kuishia Atlantiki mpakani na Namibia.
- kuelekea magharibi ni mito midogo tu
- Zambezi ikitokea kaskazini inapita karibu na Nyanda za Juu za Bie na kupokea sehemu ya maji yake hapa.
Mji mkubwa katika eneo ni Huambo (zamani: Lisbon mpya)