Nyanda za juu za Yunnan–Guizhou

Nyanda za juu za Yunnan-Guizhou ni eneo katika kusini magharibi ya China. Kanda hii inaenea hasa katika majimbo ya Yunnan na Guizhou.

Eneo la nyanda za juu za Yunnan Guizhou.

Upande wa kusini tabia yake ni zaidi kama tambarare ya juu lakini kaskazini kuna milima. Kwa jumla zinapakana na nyanda za juu za Tibet upande wa magharibi-kaskazini.

Jiografia

hariri
 
Shilin (Msitu wa miamba), Yunnan

Kwa jumla nyanda za juu huwa kwenye kimo cha mita 1,000 hadi 2,000 juu ya usawa wa bahari. Kwa muda mrefu eneo hilo limezingatiwa kuwa nyuma kiutamaduni na kiuchumi nchini China. [1] Wakazi wengi wanaishi kwa mtindo wa jadi katika vijiji.

Nyanda hizo zinatenganisha mabeseni ya mito mikubwa kama vile Yangzte, Xi Jiang na Yuan Jiang.[2] [3]

Tanbihi

hariri
  1. China's Southwest. Lonely Planet. 2007. ISBN 9781741041859.
  2. Atlas of China. Beijing, China: SinoMaps Press. 2006. ISBN 9787503141782.
  3. Suettinger, Robert Lee. "Yunnan". Encyclopædia Britannica. Encyclopædia Britannica, Inc. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Yunnan–Guizhou kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.