Nyavu (kundinyota)

Nyavu (kwa Kilatini na Kiingereza Reticulum) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia yetu.

Nyota za kundinyota Nyavu (Reticulum ) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya kundinyota Nyavu

Mahali pake hariri

Nyavu lipo jirani na kundinyota za Panji (Dorado) upande wa magharibi, Saa (Horologium) upande wa mashariki na Nyoka Maji (Hydrus) upande wa kusini.

Jina hariri

Nyavu ni kati ya makundinyota yaliyobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama ilivyo kwa kundinyota kama ilivyo kwa nyota nyingine nyingine zinazoonekana kutoka nusutufe ya kusini pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nazo. Kundinyota hii ilielezwa mara ya kwanza na wanaastronomia Wajerumani katika karne ya 17 kwa jina “Rhombus” (sambamba sawa); Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 alii kwa jina “Réticule Rhomboide “ akitaja mistari katika lensijicho ya darubini yake.

Lacaille alikaa miaka miwili kwenye Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) akitazama nyota za anga ya kusini ambazo wakati ule zilianza tu kujulikana kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Alipima nyota 10,000 akazipanga katika kundinyota na kutunga majina kwa kundinyota mpya 14[2]. Jina la Kifaransa lilitafsiriwa kwa Kilatini na kufupishwa kama "Reticulum“(Nyavu).

Chaguo la jina lilikuwa dalili ya kipindi cha Zama za Mwangaza ambapo Lacaille alitumia majina ya zana za siku zake kwa kutaja nyota, si tena majina ya mitholojia ya kale.

Nyavu ipo kati ya makundinyota 88 yanayoorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3] kwa jina la Reticulum. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Ret'.[4]

Nyota hariri

Nyota za Nyavu ni chache na dhaifu; angavu zaidi ni Alpha Reticuli yenye mwangaza unaoonekana wa mag 3.3 ikiwa umbali wa miakanuru 162 kutoka Dunianini [5]. Beta Reticuli huwa na mag 3.84[6].


Tanbihi hariri

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Reticulum " katika lugha ya Kilatini ni "Reticuli" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Reticuli, nk.
  2. Histoire de l'Académie royale des sciences ; taarifa ya Lacaille katika "Historia ya Akademia ya Kifalme ya sayansi", uk. 588, Tovuti ya Bibliothèque nationale de France (BnF), iliangaliwa Julai 2017
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  5. ALPHA RET (Alpha Reticuli), tovuti ya Jim Kaler, Prof. Emeritus of Astronomy, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
  6. bet Ret, tovuti ya Simbad, Chuo kikuu cha Strasbourg, iliangaliwa Oktoba 2017

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyavu (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.