Nyeri
Nyeri ni mji wa Kenya ya kati, takriban kilomita 100 kaskazini kwa Nairobi, miguuni mwa safu ya Aberdare ikitazama mlima Kenya. Nyeri ni makao makuu ya Kaunti ya Nyeri.
Nyeri | |
Mahali pa mji wa Nyeri katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°25′0″S 36°57′0″E / 0.41667°S 36.95000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | |
Nyeri | |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 125,357 |
Mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 125,357[1]. Wakazi walio wengi ni Wakikuyu.
Nyeri imejulikana kimataifa kwa sababu ni mahali pa kuzikwa kwa Robert Baden-Powell anayekumbukwa kama mwanzilishi wa harakati ya maskauti. Maskauti kutoka nchi mbalimbali za dunia hufika hapo mara kwa mara kwa kumheshimu mzee huyu.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |