Nyimbo za jadi
Nyimbo za jadi ni nyimbo zinazoimbwa na watu wa kabila fulani kama sehemu ya utamaduni wao. Jamii huimba nyimbo hizo kama sehemu ya utamaduni wao lakini pia huwaburudisha kutokana na staili zao za uchezaji na hata uimbaji pia. Nyimbo za asili zina umuhimu mkubwa katika maisha kwani humfanya mtu afurahie kwa kuwa katika kabila lenye nyimbo nzuri na za kuvutia.
Kwa mfano Tanzania kuna makabila yanayoadhimisha na kuimba nyimbo hizo: Wamakonde huimba sindimba, Wapogoro huimba sangura n.k. Makabila mbalimbali huimba nyimbo hizo kwa lengo la kuburudika, kufurahia jambo n.k.
Faida ya kuimba nyimbo za asili
hariri- 1) Kuburudisha jamii
- 2) Kudumisha utamaduni wa jamii husika
- 3) Ni utambulisho wa jamii na taifa ambapo mtu huweza kumtambua kutokana na anavyoimba
- 4) Kuelimisha jamii
- 5) Kutumika katika kuwaenzi viongozi wao
- 6) Kutolea mafunzo kwa wengine
Lini nyimbo za asili zinapoimbwa
hariri- 1) Wakati wa kuwakaribisha wageni
- 2) Wakati wa sherehe za unyago na jando
- 3) Wakati watu wanapooana
- 4) Wakati wa kazi na baada ya kazi ili kufanya imalizike kwa urahisi
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyimbo za jadi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |