Nyuki-asali
Nyuki-asali anayekusanya mbelewele
Nyuki-asali anayekusanya mbelewele
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Familia: Apidae (Wadudu walio na mnasaba na nyuki)
Nusufamilia: Apinae
Jenasi: Apis
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Spishi 7

Nyuki-asali ni aina za nyuki wa kabila Apini katika familia Apidae ambao hutengeneza asali na kuiweka katika sega za nta.

Nyuki-asali hufugwa sana kila mahali duniani lakini wengine wanaishi porini na asali yao hukusanywa kwa kuvunja mizinga yao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unaendelea kupanuka.

Wadudu wa kijamii

hariri

Nyuki-asali ni wadudu wa kijamii maana yake wanaishi katika makundi si peke yao kama aina nyingine za nyuki. Wanajenga sega ya nta ndani ya mzinga wa nyuki na humu hutunza asali yao.

Kuna aina tatu za nyuki ndani ya kundi hili nao ni:

  • malkia wa nyuki ni mama wa nyuki wote ndani ya kundi na kazi yake ni kutaga mayai pekee
  • nyuki wafanyakazi ni wakazi wengi wa mzinga na wote ni wa kike. Ni hao wanaofanya kazi yote kama kukusanya mbelewele na mbochi, kusafisha mzinga, kutengeneza nta, kujenga sega, kumlisha malkia na majana, kulinda mzinga
  • nyuki wa kiume au wadudume ni wachache na kazi yao ya pekee ni kumpanda malkia ambaye si yule wa mzinga wake kwa kawaida; baadaye wanafukuzwa kwenye mzinga na hawapewi chakula tena

Spishi na nususpishi za Afrika

hariri

Spishi za Asia

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyuki-asali kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.