Ogani ni sehemu ya mwili au mmea inayofanya kazi fulani ya pekee.

Ogani huundwa na seli maalumu zilizopo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo maalumu ya ogani husika.

Mifano ya ogani za binadamu (pamoja na wanyama wengi kwa jumla) ni moyo, mapafu, ini na kadhalika.

Ogani za binadamu hariri

Idadi zinatajwa kwa binadamu mwenye umri wa miaka 20-30, urefu wa sentimita 170, uzani wa kilogramu 70.

Sehemu ya mwili uzito asilimia ya masi ya mwili
Musuli 30,0 kg 43,0 %
Kiunzi cha mifupa bila uboho 7,0 kg 10,0 %
Ngozi 6,1 kg 8,7 %
Damu 5,4 kg 7,7 %
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula 2,0 kg 2,9 %
Ini 1,7 kg 2,4 %
Uboho 1,5 kg 2,1 %
Ubongo 1,3 kg 1,8 %
Mapafu 1,0 kg 1,4 %
Moyo 0,3 kg 0,43 %
Mafigo 0,3 kg 0,43 %
Tezi la koromeo 0,02 kg 0,03 %
Wengu 0,18 kg 0,26 %
Jumla 70 kg 100 %
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ogani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.