Olaratumab, inayouzwa kwa jina la chapa Lartruvo, ilikuwa ni dawa iliyotumika kutibu aina fulani ya uvimbe unaotokana na saratani unaotokea katika tishu laini (soft tissue sarcoma). Haipendekezwi kwa sababu haina faida tena. Dawa hii ilikuwa ikitolewa kwa njia ya sindano kwenye mshipa.

Olaratumab ?
Monoclonal antibody
Aina Whole antibody
Chanzo Binadamu
Lengo PDGF-R α
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Lartruvo
AHFS/Drugs.com Monograph
Taarifa za leseni EMA:[[[:Kigezo:EMA-EPAR]] Link]US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito ?
Hali ya kisheria POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Kuingizwa kwa mishipa
Data ya utendakazi
Kufunga kwa protini Hakuna
Kimetaboliki Vimeng'enya vya protini
Nusu uhai Siku kumi na moja
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe IMC-3G3, LY-3012207
Data ya kikemikali
Fomyula C6554H10076N1736O2048S40 
 N(hii ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida yalijumuisha kichefuchefu, uchovu, chembechembe za chini za damu nyeupe, maumivu, chembechembe kidogo za damu ya platleti, maumivu ya tumbo, potasiamu kidogo, maumivu ya kichwa, uvimbe na athari za mzio.Dawa hii ni kingamwili ya monokloni ambayo huzuia kipokezi cha sababu ya ukuaji kinachotokana na chembe chembe za alpha.

Olaratumab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2016.[1] Mnamo mwaka wa 2019, iliondolewa sokoni kwa sababu haikuwa na faida tena. Iliuzwa kwa takriban dola 2,600 kwa miligramu 500 nchini Marekani.[2]

Marejeo

hariri
  1. "Lartruvo". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Septemba 2020. Iliwekwa mnamo 7 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Lartruvo Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 7 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)