Omidenepagi
Omidenepagi (Omidenepag), inayouzwa kwa jina la chapa Eybelis miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu shinikizo la juu la damu la macho ikiwa ni pamoja na glaukoma.[1][2] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhisi kuathirika na mwanga, kutoona vizuri, uwekundu wa macho, maumivu ya kichwa na maumivu ya macho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha mabadiliko ya kope na uvimbe wa seli za jicho.[1] Ni kiamsha kipokezi cha prostaglandini E2 (EP2) ambacho huchagua kwa kiasi fulani.[1]
Omidenepagi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Japani mwaka wa 2018[2], na Marekani mwaka wa 2022.[1] Kwa sasa, haijakuwa katika mchakato wa kuidhinishwa si Ulaya wala Uingereza kufikia mwaka wa 2022.[3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Omlonti- omidenepag isopropyl solution/ drops". DailyMed. 30 Septemba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Oktoba 2022. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 Duggan S (Desemba 2018). "Omidenepag Isopropyl Ophthalmic Solution 0.002%: First Global Approval". Drugs. 78 (18): 1925–1929. doi:10.1007/s40265-018-1016-1. PMID 30465134.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Omidenepag isopropyl". SPS - Specialist Pharmacy Service. 30 Septemba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Oktoba 2022. Iliwekwa mnamo 16 Desemba 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Omidenepagi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |