Osimertinib, inayouzwa kwa jina la chapa Tagrisso, ni dawa inayotumika kutibu saratani ya mapafu isiyo ya seli ndogo (non-small-cell lung cancer) kwa mabadiliko fulani katika jeni ya EGFR (kipokezi cha sababu ya ukuaji wa ngozi).[1] Dawa hii inachukuliwa kwa njia ya mdomo.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara, upele, uchungu mdomoni, uchovu na kuvimba kwa ini.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha nimonia, kuongeza muda wa QT (ugonjwa wa mdundo wa moyo unaoweza kusababisha mapigo ya moyo ya haraka na yenye fujo), ugonjwa wa moyo na kuvimba kwa macho.[2] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[2] Dawa hii ni kizuizi cha tyrosine kinase.[2]

Osimertinib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2015 na Ulaya mwaka wa 2016.[2] [1] Nchini Uingereza inagharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £5,800 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[3] Nchini Marekani kiasi hiki kinagharimu takriban dola 16,000 za Kimarekani.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 "Tagrisso EPAR". European Medicines Agency (EMA). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Osimertinib Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1038. ISBN 978-0857114105.
  4. "Tagrisso Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Osimertinib kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.