Papa Fabian

Papa Fabian alikuwa Papa kuanzia mwaka 236 hadi kifodini chake tarehe 20 Januari 250[1]. Alitokea Roma, Italia.

Papa Fabian na Mtakatifu Sebastian.

Alimfuata Papa Antero akafuatwa na Papa Kornelio.

Kadiri ya wanahistoria Wakristo[2], chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 20 Januari[3].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. The Vetus Martyrologium Romanum (1961) under Die 18 Decembris: Quintodecimo Kalendas Januarii: "Turonis, in Gallia, Sancti Gatiani Episcopi, qui, a Sancto Fabiano Papa primus ejusdem civitatis Episcopus ordinatus est, et multis clarus miracolis obdormivit in Domino".
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Fabian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.