Papa Martin I

Papa Martin I alikuwa Papa kuanzia tarehe 5 Julai 649 hadi kifodini chake tarehe 16 Septemba 655[1]. Alitokea Todi, Umbria, Italia[2].

Mt. Martino I.

Alimfuata Papa Theodor I akafuatwa na Papa Eugenio I.

Baada ya kuwa balozi wa Papa Theodori I huko Konstantinopoli, alichaguliwa kuwa mwandamizi wake bila kibali cha kaisari wa Dola la Roma Mashariki.

Kwa kuwa katika Mtaguso wa Laterano (649) na baada yake alipinga uzushi ulioungwa mkono na kaisari Konstans II, wa kwamba Yesu alikuwa na utashi wa Kimungu tu, bila ule wa kibinadamu, hatimaye alikamatwa na kupelekwa uhamishoni sehemu za Ukraina kusini, alipofariki[3].

Ndiyo sababu tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 13 Aprili[4].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Martin I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.