Paradiso (kutoka Kiajemi: پردیس, bustani) ni jina la mahali pa amani kamili palipo tarajio kuu la waumini wa dini mbalimbali.

Nicolas Poussin, Majira ya kuchipua katika mfululizo wa Majira manne ya paradiso, 16601664.
Paradiso kadiri ya Jan Bruegel.

Dini za Abrahamu zinatumia jina hilo kwa Eden, yaani ulimwengu wa kabla ya dhambi ya asili, na vilevile kwa ule unaotarajiwa kuwepo milele.

Asili ya jinaEdit

Neno "paradiso" limeenea katika lugha nyingi (paradis, paradisus, paradise n.k.) kupitia Kigiriki parádeisos (παράδεισος), kutoka Kiajemi cha zamani *paridayda- "eneo lililozungukwa na uzio".

Katika Agano la KaleEdit

Katika Kiebrania פרדס (pardes) inapatikana mara tatu katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania): Wimbo Ulio Bora 4:13, Mhubiri 2:5 na Nehemia 2:8.

Katika Agano JipyaEdit

Katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo neno linapatikana vilevile mara tatu: Luka 23:43 (Yesu msalabani alilitumia akimjibu mhalifu aliyetubu ili kumhakikishia watakuwa pamoja), 2 Kor 12:4 (Mtume Paulo alilitumia kuelezea hali ya pekee aliyojaliwa kwa njozi, Ufunuo 2:7 (kuhusiana na Kitabu cha Mwanzo 2:8 na mti wa uzima.

Katika UislamuEdit

Kwa Kiarabu na katika Quran inaitwa فردوس., firdaus.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paradiso kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.