Parts per million ni jina kutoka lugha ya Kiingereza lenye maana "sehemu za milioni" kwa hiyo inalingana na namba 10−6. Kifupi chake ni ppm kinatumiwa kutaja kiwango cha dutu katika jumla fulani. Kwa hiyo matumizi ya "ppm" yanalingana na "asilimia" inayomaanisha "sehemu za mia" au 10−2.

Matumizi hariri

Kizio cha ppm hutumiwa katika vipimo vya kemia. Ppm inaweza kutajwa pia kama miligramu katika masi ya kilogramu moja, au mililita katika mita ya ujazo.

Kwa mfano hutumiwa kutaja kiasi cha machafuko yaliyobaki katika dutu baada ya kuisafisha.

Katika elimu ya hifadhi ya mazingira mara nyingi viwango vya ppm vya gesi fulani au machafuko mengine katika hewa au maji ni vipimo muhimu kuamulia hatari za machafuko.