Pathojeni

Pathojeni (ing. pathogen, kutoka gir. πάθος pathos “mateso” na -γενής -genēs “kuzaa”) au kiambukizi ni kile kinachosababisha ugonjwa. Kwa kawaida ni vidubini kama vile bakteria, virusi, fungi au vimelea vinavzoweza kusababisha magonjwa.

Si kila bakteria au fungi inasababisha ugonjwa, kinyume chake tunaishi kwa kuwa na mamilioni ya bakteria katika utumbo ambazo ni lazima kuwepo kwa afya yetu. Vidubini hivi vyote ni vidogo mno, havionekani kwa macho.

Hasara kutokana na pathojeniEdit

Athira hatari ya vidubini ni hasa tatu zifuatazo:

  • vinaharibu tishu kwa kula seli za mwili (phagocytosis)
  • vinasababisha mjibizo mkali wa kingamwili, hasa homa ya juu inayoweza kuhatarisha maisha
  • vinatoa dutu zinazosababisha uharibifu mwilini

Bakteria zinaleta hasara kwa kutoa dutu ambazo ni sumu mwilini

Kingamwili dhidi ya pathojeniEdit

Mwili una mbinu mbalimbali kujitetea dhidi za pathojeni. Hasa mfumo wa kingamwili unatambua na kuondoa pathojeni. Kuna pia bakteria kadhaa zinazoishi mwilini (kwa mfano tumboni) zinazoweza kupigana na pathojeni kadhaa. Lakini kama mfumo wa kingamwili umedhoofishwa kwa mfano kwa ambukizo ya UKIMWI au kutibiwa kwa madawa ya antibiotika bakteria za kigeni zinaweza kuongezeka na kuleta hasara.