Peter Tosh (19 Oktoba 194411 Septemba 1987) huyu alikuwa ni mwanamuziki Mjamaika wa mtindo wa rege, alikuwa na kipaji mahiri cha kutunga mashairi ya muziki, pia alikuwa ni mpigaji mahiri wa gitaa.

Peter Tosh, 1978

Peter alizaliwa tarehe 19 Oktoba 1944, akiwa ni mtoto pekee wa mama Alvera Coke, baba yake aliitwa James Mclntosh ambaye alikuwa ni mhubiri wa kanisa la Savanna-la-mar. Peter ni jina ambalo alibadilisha lakini jina lake halisi ni Winston Hubert Mclntosh. Katika maisha yake hakubahatika kulelewa na baba na mama yake, alilelewa na shangazi yake sababu wazazi wake hawakuwa na muda wa kumlea, hivyo huwezi kuamini alijitunza mwenyewe kwa baadhi ya mambo bila kupata matunzo kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa ni baba wa watoto wengi.

Peter alianza kupiga ala za muziki akiwa kijana wa umri mdogo, alijifunza kupiga kinanda kwa miezi sita pia alijifunza kupiga gitaa, ala hiyo ndiyo iliyo kuja kumpa umaarufu, mwaka 1956 baada ya kuondoka Savanna-la-mar Peter na shangazi yake walikwenda mji wa Denham katika jiji la Kingston, Peter alipofikia umri wa miaka kumi na tano shangazi yake alifariki, hivyo alikwenda kwa mjomba wake West Road huko Trench Town. Peter alikutana na Robert Nesta Marley (Bob Marley) na Neville O'Reilly Livingston (Bunny Wailer) na wakajiunda kuwa watatu wa kwanza wa Wailer halisi na wakajiita Wailin'Wailers, na walianza kuimba pamoja mwaka 1962 na alikuwa ni yeye tu kati yao aliyeweza kupiga ala, hivyo alifanya bidii ya kuwafundisha wenzake na alikuwa ni mmojawapo aliyemfundisha Bob kupiga gitaa. Peter alijitoa Wailers mwaka 1974 hii ni baada ya Chris Blackwell kukataa kutoa albamu yake ya kwanza yeye akiongoza safu ya uimbaji.

Peter Tosh aliuawa nyumbani kwake mwaka 1987.

Viungo vya Nje

hariri