Peter Yorke
Mwanamapinduzi wa Ireland
Peter Christopher Yorke (13 Agosti 1864 – 4 Aprili 1925) alikuwa kasisi wa Kanisa Katolikikutoka Ireland na mwanaharakati wa Jamhuri ya Ireland na haki za wafanyakazi huko San Francisco nchini Marekani.[1]
Maisha ya awali
haririPeter Christopher Yorke alizaliwa kwenye eneo la Long Walk huko Galway tarehe 13 Agosti 1864. Alikuwa mtoto wa mwisho wa Gregory Yorke, nahodha wa meli, na mke wake Bridget, aliyekuwa kwa jina la awali Kelly.[2] Gregory Yorke alifariki miezi sita kabla ya kuzaliwa kwa Peter.
Familia ya Yorke asili yao ni kutoka Uholanzi, ambapo jina lao lilikuwa linatamkwa Jorke. Babu yake Peter, Christopher Yorke, alifika Galway mwanzoni mwa karne ya 19, akijenga taa za baharini na vizuizi vya mawimbi katika maeneo ya Galway, Aran, na Westport.[3]
Marejeo
hariri- ↑ James P. Walsh and Timothy Foley, Father Peter C. Yorke Irish-American Leader, Studia Hibernica, No. 14 (1974), pp. 90–103
- ↑ "General Registrar's Office". IrishGenealogy.ie. Iliwekwa mnamo 15 Agosti 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ The Long Walk Archived 16 Agosti 2017 at the Wayback Machine., 18 July 2002
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |