Chawa
Chawa wa kichwa (Pediculus humanus capitis)
Chawa wa kichwa (Pediculus humanus capitis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Linnaeus, 1758
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Lang, 1888
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Psocodea
Nusuoda: Troctomorpha
Ngazi za chini

Familia za juu 4:

Chawa ni wadudu wadogo wa oda ndogo Phthiraptera katika nusuoda Troctomorpha wa oda Psocodea. Wahenga wao ni chawa-vitabu na kama hawa chawa hawana mabawa. Wadudu hawa wote ni vidusia wa nje juu ya ndege na mamalia isipokuwa Monotremata (kinyamadege na mhanganungu), popo, nyangumi, pomboo na kakakuona. Kuna aina mbili za chawa: wanaokula nywele, manyoya na seli za ngozi zilizokufa, na wanaofyunza damu ya mwenyeji. Chawa wa aina ya kwanza wana vipande vya mdomo vya kutafuna, wale wengine wana mdomo wa kufyunza. Miguu inabeba aina za magando madogo ili kushika nywele au manyoya ya mwenyeji. Kwa kawaida mayai ya chawa yamegandia nywele au manyoya, au pengine yamewekwa ndani ya shina la unyoya.

Binadamu ni kidusiwa wa spishi mbili: chawa wa binadamu (Pediculus humanus) na chawa-kinenani (Pthirus pubis). P. humanus imegawanya katika nususpishi mbili kufuatana na sehemu ya mwili ambapo zinakaa: chawa-kichwani (P. h. capitis) na chawa-mwilini (P. h. humanus). Chawa wa binadamu wana uhusiano wa karibu na chawa wanaopatikana kwenye sokwe mtu wa kawaida na bonobo, hata hivyo chawa-kinena wako karibu zaidi na chawa wa ngagi. Ingawa chawa wa binadamu wanafikiriwa kuwa waligeua tangu wanadamu watengane na sokwe mtu, chawa-kinenani wanaonekana kuwa waliambukiza wanadamu katika hatua za baadaye za mageuzi yao, yumkini wakati wa kulala kwenye viota vya ngagi au wakati wa kuwachinja, na kutengana na chawa wa ngagi.

Uharibifu wa chawa na jinsi ya kumuangamiza hariri

Chawa-kichwani hawasababishi magonjwa lakini chawa-mwilini husababisha magonjwa, kama milipuko ya kuhara damu, homa ya kuchamka na homa ya mitaro ya vita. Hata hivyo, katika jamii nyingi, chawa huonekana kuwa kero na ishara kwamba mbebaji ni mchafu au anaishi katika uchafu. Pia humfanya mtu kuwa dhaifu kutokana na kufyonzwa kwa damu.

Kuna dawa kadhaa za kupuliza ili kuwaua wadudu hawa. Usafi pia ni muhimu kama wataka kuwakwepa.

Picha hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chawa kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.