Pirfenidone, inayouzwa kwa jina la chapa Pirespa miongoni mwa zingine, ni dawa inayotumika kutibu fibrosisi ya mapafu isiyoeleweka chanzo chake.[1] Dawa hii inatumika kwa ugonjwa wa chini na wa wastani[2] na inachukuliwa kwa njia ya mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, upele, uchovu, kiungulia, maumivu ya kichwa na kuchomwa na jua.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya ini.[3] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[4] Jinsi inavyofanya kazi si wazi kabisa, hata hivyo inapunguza uzalishaji wa seli ambazo zina jukumu muhimu katika uponyaji wa vidonda na uundaji wa tishu unganishi mwilini (fibroblasts).[1]

Pirfenidone iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu huko Uropa mnamo mwaka wa 2011 na Amerika mnamo mwaka wa 2014.[1][3] Nchini Uingereza wiki 4 za matumizi ya dawa hii hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £2,000 kufikia mwaka wa 2021.[2] Nchini Marekani, kiasi hiki ni takriban dola 9,900 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Esbriet". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 314. ISBN 978-0857114105.
  3. 3.0 3.1 "Pirfenidone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Pirfenidone (Esbriet) Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Esbriet Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 28 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pirfenidone kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.