Poractant alfa, inayouzwa kwa jina la chapa Curosurf miongoni mwa nyinginezo, ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia matatizo ya kupumua (RDS) kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.[1][2] Dawa hii inapunguza hatari ya kifo na hali ya hewa kuvuja na kuingia kwenye nafasi ya kati ya mapafu na ukuta wa kifua (pneumothoraces)[2] na inatolewa kwenye koo la hewa (trakea).[1]

Poractant alfa
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Curosurf
AHFS/Drugs.com Kigezo:Drugs.com
Kategoria ya ujauzito N
Hali ya kisheria -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Ndani ya trakea
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula ?

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mapigo ya moyo polepole, shinikizo la chini la damu na oksijeni ya chini.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuziba kwa mirija ya koo la hewa.[1] Dawa hii inaundwa kwa kemikali ya kuzuia mvutano wa mapafu (pulmonary surfactant) ambayo zimeundwa kwa mafuta ya fosforasi (phospholipids) na protini za kuzuia mvutano.[1]

Dawa hii iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1999.[1] Nchini Marekani, iligharimu takriban dola 1,000 kwa mililita tatu kufikia mwaka wa 2021.[3] Dawa hii inatengenezwa kutoka kwa mapafu ya nguruwe.[1]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Poractant Alfa Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "DailyMed - CUROSURF- poractant alfa suspension". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Curosurf Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)