Pori la Akiba la Sabi Sand

Hifadhi ya Sabi Sand iko karibu na Mbuga ya Kitaifa ya Kruger huko Lowveld ya Mpumalanga, Afrika Kusini[1]. Rasmi liliitwa Sabi Sand Wildtuin,Pori la Akiba la Sabi Sand lina kundi la mapori ya akiba binafsi. Lango la Newington liko 24°52′9″S 31°24′16″E na magharibi mwa Lango la Kruger na kambi ya Skukuza ya Kruger Park. Milango mingine ni lango la Gowrie upande wa kaskazini na lango la Shaws upande wa kusini.

Simba dume na mtoto wake wakila nyati huko Kaskazini mwa Pori la Sabi
Simba dume na mtoto wake wakila nyati huko Kaskazini mwa Pori la Sabi

Jina la hifadhi hii linatokana na Mto Sabie kwenye mpaka wake wa kusini na Mto Sand unaopita humo. Eneo la hifadhi hiyo ni hekta 62,308 (623.08 km2)[2] na inashiriki mpaka usio na uzio wa kilomita 50 (31 mi) na Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger upande wake wa mashariki.

Hifadhi ya Sabi Sands hujumuisha Buffelshoek, Djuma, Uwanda wa Tembo, Uwanda wa Duma, Mala Mala, Chitwa Chitwa, Nkorho, Simbambilli, Arathusa, Londolozi, Umkumbe, Nottens, Sabi Sabi, Lion Sands, Kirkman's Kamp, Singita, Exeter Leadwood, Inyati, Idube, Dulini, Leopard Hills, Savanna na Ulusaba[3].

Marejeo;

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-09. Iliwekwa mnamo 2022-06-11. 
  2. "History of Sabi Sands Game Reserve, South Africa". southafrica.co.za. Iliwekwa mnamo 2022-06-11. 
  3. "https://sabi.krugerpark.co.za/sabi-sand-map.html". sabi.krugerpark.co.za. Iliwekwa mnamo 2022-06-11.