Poxi Presha
Poxi Presha (1971 - 2005), jina halisi Prechard Pouka Olang, alikuwa mwanzilishi wa muziki wa aina ya rap nchini Kenya. Alijitokeza katikati ya miaka za tisaini na miziki wa hip hop ya ulioimbwa katika lugha ya Dholuo .[1] Albamu yake ya kwanza Total Balaa ilitolewa mwaka wa 1999, na ilikuwa imetangulia na magoma katika redio kama "dhako", "Mummy" na "Otonglo Time". Albamu hii ilifuatiwa na ingine Vita Kwaliti .[2]
Alikuwa pia ni MC wa kundi la Nairobi City Ensemble, ambalo ndilo lilitoa albamu ya "Kaboum Boum", ilokuwa na mrudio wa wimbo wa "Lunchtime", awali wimbo huo maarufu ulikuwa umeimbwa na mwimbaji wa benga Gabriel Omolo.
Alijulikana kama "kijana mbaya wa muziki wa Kenya " kutokana na idadi ya matukio, kama vile kukosana na watayarishaji wake Bruce Odhiambo na Tedd Yosia. Alitoa wimbo wa mchongoanao "Wape Really?" ukilenga watayarishaji na mapromota.
Katika miaka yake ya baadaye, Poxi Presha alifanya kazi kama mwanaharakati wa kupinga kunakili kazi ya wasanii bila idhini yao.
Poxi Presha alizaliwa mjini Mombasa lakini makao yake yalikuwa mjini Nairobi wakati wa uimbaji yake. Alifariki katika Hospitali ya St Mary's katika Langata, Nairobi tarehe 14 Oktoba 2005 kutokana na kifua kikuu, akiwa na umri wa miaka 34 .
Marejeo
hariri- ↑ New Internationalist, Aprili 2001 Translate this!
- ↑ "Poxi Presha website through archive.org". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-12-04. Iliwekwa mnamo 2004-12-04.