Pregaluxmi "Pregs" Govender (alizaliwa 15 Februari 1960) ni mwanasiasa wa kike kutoka nchini Afrika Kusini, mwanaharakati wa haki za binadamu na mwandishi.

Pregaluxmi Pregs Govender (2017)

Maisha hariri

Alizaliwa 1960 mjini Durban, Afrika Kusini. Baba yake alikuwa mwandishi, mama alikuwa mwalimu. Ilhali familia iliainishwa kuwa "Wahindi" chini ya sheria za apartheid (ubaguzi wa rangi), ilipaswa kuondoka kwao na kuhamia katika sehemu iliyotengwa kwa kundi lao. Alianza kuelewa na kupinga ubaguzi alipokuwa na umri wa miaka 14 akajiunga na chama cha ANC wakati bado ilikuwa imepigwa marufuku. Akiendelea na masomo alihitimu Chuo Kikuu cha Durban-Westville akawa mwalimu wa Kiingereza na (UDW, now the University of KwaZulu-Natal – UKZN), na kuwa mwalimu wa Kinngereza shuleni akiendelea kufanya kazi chuoni. 1987 aliajiriwa na chama cha wafanyakazi wa nguo (Garment Workers Industrial Union GWIU) akiogoza idara ya elimu ya chama kilichokuwa na wanachama wa kike wengi. [1] Wakati utawala wa apartheid ulianza kuporomoka, aliongoza Ushirikiano wa Kitaifa wa Wanawake (Women’s National Coalition WNC) uliopigania haki za wanawake. Kwenye uchaguzi huru wa kwanza mwaka 1994 alichaguliwa mbunge akiwa mgombea wa chama cha ANC,

Kazi katika Bunge la Afrika Kusini (1994-2002) hariri

Mnamo mwaka 1996, Govender alikuwa mhariri wa ripoti ya Afrika Kusini kwenye Mkutano wa Dunia wa Wanawake 1995 mjini Beijing. Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa bunge na pia kamati ya kusimamia uboreshaji wa maisha ya wanawake nchini (JMCIQLSW). Wakati wa kipindi chake (1996-2002),JMCIQLSW iliweza kupeleka sheria mbalimbali bungeni zilizokubaliwa, kama vile Sheria dhdi ya Ukatili wa Nyumbani [2], Sheria ya Utambuzi wa Ndoa za Kimila, 1998, Sheria ya Utunzaji wa Watoto[3] pamoja sheria za kuboresha haki za wanawake kwenye maeneo ya kazi.

Mnmao mwaka 2000 idadi ya wagonjwa wa UKIMWI ilikuwa imeongezeka mno nchini Afrika Kusini na wakati ule rais Thabo Mbeki alikataa kuona uhusiano baina ya virusi na ugonjwa. Alipokataa kununua madawa ya kudhibiti virusi vya UKIMWI, Govender alikosoa waziwazi msimamo huo na hatimaye kujiuzulu bungeni.

Mwandishi wa habari Mark Gevisser alielezea mnamo 2007 : "Mbunge mmoja tu wa ANC, Pregs Govender, mwenyekiti wa kamati ya bunge juu ya hadhi ya wanawake, alijiuzulu na kumkosoa Mbeki hadharani. Na hata nyuma ya milango iliyofungwa ni mtu mmoja au wawili tu ndio walikuwa na ujasiri wa kumwambia Mbeki walidhani alikuwa amekosea.[4] "

Kamati ya Utathmini wa Bunge na Tume la Haki za Binadamu hariri

Mnamo mwaka 2007 Govender alichaguliwa mwenyekiti wa Kamati ya Utathmini wa Bunge iliyotoa taarifa juu ya kazi ya bunge.

Kuanzia mwaka 2009 hadi 2015 aliteuliwa kuwa kamishna wa Tume la Haki za Binadamu la Afrika Kusini na kuwa makamu wa mwenyekiti wake[5].


Marejeo hariri

  1. Pregaluxmi (Pregs) Govender, tovuti ya South African History Online
  2. Domestic Violence Act
  3. Child Maintenance Act
  4. Mbeki admits he is still Aids dissident six years on, gazeti lla Guardian (UK), tar. 6 Novemba 2007
  5. Time to guard the guardians, tovuti ya South Africa Human Rights Commission