Programu za Fulbright za Mabadilishano

Shirika la Fulbright ni shirika ambalo lilianzishwa katika nchi ya Marekani na lina programu nyingi kwa wanafunzi na walimu. Nia ya programu zote za Fulbright ni kuhimiza amani, ufahamu, na ushirikiano kati ya nchi zote katika dunia.[1]

Nembo ya Programu ya Fulbright.
Seneta J. William Fulbright, mtu ambaye alipendekeza Programu ya Fulbright.

Historia ya Fulbright

hariri

Katika mwaka 1946, programu ya Fulbright ilipendekezwa katika nchi ya Marekani na seneta J. William Fulbright na ilitiwa saini na Rais Harry Truman. Sasa, nchi mia moja na sitini zinafanya programu ya Fulbright[1], na nchi arobaini na tisa kati ya nchi hizo zina tume zao wenyewe za Programu ya Fulbright.[2] Kila mwaka, takriban watu elfu nane wanapata tuzo ya Fulbright. Tangu mwaka ambao programu ya Fulbright ilipoanzishwa, takribani watu laki nne wamefaidika programu ya Fulbright.[1]

Programu ya Msaidizi wa Kufundisha Lugha ya Kigeni (FLTA)

hariri

Programu ya Msaidizi wa Kufundisha Lugha ya Kigeni (FLTA) ni programu ambayo inafadhiliwa na Ofisi ya Masuala ya Elimu na Utamaduni ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Programu hii ina lugha thelathini na tano kutoka nchi hamsini na tano, na watu wanaotoka moja ya nchi hizi wanaweza kufanya programu ya FLTA.[3]

Programu hii inafanyika kwa ajili ya mabadilishano ya utamaduni na lugha. Katika programu hii, walimu wa nchi nyingine wanaweza kuja Marekani ili kuwafundisha wanafunzi Wamarekani kuhusu lugha ya mataifa yao. Washiriki wanakuwa wasaidizi wa kufundisha lugha na utamaduni katika vyuo vikuu wanapopelekwa. Programu hii ya Fulbright inalenga kuendeleza ufundishaji wa lugha ambazo hazifundushwi kwa wingi.[3] Kwa mabadilishano, wasaidizi wa kufundisha wanajifunza kuhusu utamaduni wa nchi ya Marekani wakati wanapoishi pale. Pia, wanapata fursa ya kuendeleza ustadi wa kufundisha lugha ya kigeni.[2]

 
Nchi za Afrika Mashariki ambazo zina programu za FLTA.

Programu ya FLTA Katika Bara la Afrika

hariri

Sasa, kuna programu za Fulbright katika nchi mia moja na sitini katika dunia. Katika bara la Afrika, nchi za Kenya, Nigeria, Senegal, Afrika Kusini, na Tanzania zina programu ya FLTA.[3] Baadhi ya lugha za Afrika ambazo Programu ya FLTA inafundisha ni Kiarabu, Kiswahili, Kiwolof, Kiyoruba, na Kizulu.[4] Katika Afrika Mashariki, nchi za Kenya na Tanzania zina programu za Fulbright za FLTA ili kufundisha Kiswahili nchini Marekani.[3]  

Mahitaji ya Programu ya FLTA kwa Waombaji

hariri

Ili kufanya programu ya FLTA, watu ambao wanataka kutuma maombi ya FLTA wanahitaji:

  • Kuwa na shahada ya Chuo Kikuu (au kiwango cha elimu kinacholingana)
  • Kuishi ndani ya nchi ambapo wanaombea na hawawezi kuwa raia wa nchi ya Marekani
  • Kusema Kiingereza kwa ufasaha
  • Kuwa na uzoefu au mafunzo kidogo ya kufundisha Kiingereza[3]

Kila nchi inaweza kuwa na vigezo vingine zaidi – waombaji wanapaswa kutafuta vigezo mahususi vya nchi zao kabla ya kutuma maombi ya programu ya FLTA.[2]

Programu Nyingine

hariri

Kwa watu wa nje ya Marekani, zaidi ya Programu ya Msaidizi wa Kufundisha Lugha ya Kigeni (FLTA), kuna Programu ya Fulbright ya Wanafunzi wa kigeni. Programu hii ni kwa wanafunzi kutoka nchi nyingine ili kufanya utafiti au kusoma katika nchi ya Marekani.[5] Pia, Fulbright ina programu zaidi kwa wanafunzi Wamarekani katika Programu ya Fulbright ya Wanafunzi Wamarekani. Kuna Programu ya Fulbright ya Kusoma/Utafiti na Programu ya Msaidizi wa Kufundisha wa Kiingereza.[6] Ili kujifunza zaidi kuhusu programu zote za Fulbright, unaweza kusoma katika tovuti ya Fulbright.

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Fulbright Program Overview | Bureau of Educational and Cultural Affairs". eca.state.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Home". exchanges.state.gov (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Foreign Fulbright Program - FLTA Program". foreign.fulbrightonline.org. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  4. University of Pennsylvania Africa Center. (n.d.). African Language Offerings. https://www.africa.upenn.edu/sites/www.africa.upenn.edu/files/African%20Language%20Offerings%20-%20AFST.pdf
  5. "Foreign Fulbright Program - Foreign Student Program". foreign.fulbrightonline.org. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.
  6. "US Fulbright Program - Types of Awards". us.fulbrightonline.org. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.