Ndegesukari

(Elekezwa kutoka Promerops)
Ndegesukari
Ndegesukari wa rasi
Ndegesukari wa rasi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Promeropidae (Ndege walio na mnasaba na ndegesukari)
Jenasi: Promerops
Brisson, 1760
Ngazi za chini

Spishi 2:

Ndegesukari (kutoka Kiing.: sugarbird) ni ndege wa familia Promeropidae. Wanatokea Afrika Kusini tu. Domo lao limepindika na mkia ni mrefu sana, kwa dume hasa. Ulimi wao ni mrefu wenye ncha kama brashi na unaweza kuchomozwa nje ili kula mbochi. Hupata nguvu yao takriban yote kutoka mbochi wa maua ya jenasi Protea na ndege hawa ni wachavushaji muhimu wa maua haya. Hula pia wadudu ambao wanavutika na maua ya Protea, kama nyuki na nzi. Hulijenga tago lao katika panda ya mti na jike huyataga mayai mawili.

Spishi za Afrika

hariri
  Makala hii kuhusu "Ndegesukari" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili sugarbird kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio ni ndegesukari.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.