Popo-matunda

(Elekezwa kutoka Pteropodidae)
Popo-matunda
Popo mwekundu (Rousettus aegyptiacus)
Popo mwekundu
(Rousettus aegyptiacus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Ngeli ya chini: Eutheria
Oda: Chiroptera (Popo)
Nusuoda: Yinpterochiroptera
Familia ya juu: Pteropodoidea (Popo-matunda)
Familia: Pteropodidae
Gray, 1821
Ngazi za chini

Nusufamilia 6:

Popo-matunda ni aina za popo wanaokula matunda hasa. Kibiolojia ni mamalia wa familia ya juu Pteropodoidea katika oda Chiroptera, wanaofanana na panya au mbwa wadogo wenye mabawa. Kwa kawaida spishi hizi ni kubwa kuliko zile za popo-wadudu (oda Yangochiroptera na familia ya juu Rhinolophoidea) lakini kuna spishi zilizo ndogo kulika spishi fulani za popo-wadudu. Yumkini spishi kubwa kabisa ni popo-mbweha wa Uhindi aliye na uzito wa kg 1.6, urefu wa mwili wa sm 40 na urefu wa mabawa wa hadi m 1.5. Mabawa ya popo-mbweha mkubwa yana urefu wa hadi m 1.6. Spishi ndogo kabisa ni popo-matunda mabawa-madoa aliye na uzito wa g 15 na urefu wa mwili wa sm 5-6. Popo-matunda hula matunda au mbochi. Wale wanaokula matunda husambaza spishi za miti na wale wanaokula mbochi huchavusha maua. Kama popo wote hata popo-matunda hukiakia usiko na hulala mchana. Wakilala wananing'inia juu chini na kujifunika kwa mabawa. Takriban spishi zote hulala mitini, lakini spishi kadhaa hulala ndani ya mapango.

Utambuaji kwa mwangwi

hariri

Kinyume na popo-wadudu, popo-matunda hawatoi sauti za marudio ya juu wakitumia kikoromeo chao ili kutambua mazingira na kutafuta chakula kwa kusikiliza miangwi ya sauti hizi, ijapokuwa spishi kadhaa za jenasi Rousettus zinaweza kupiga vidoko kwa ulimi wao. Spishi nyingine hutoa mialiko kwa mabawa yao.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri