Ukiki

Ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares, familia Cuculidae
(Elekezwa kutoka Pundamakaa)
Ukiki
Ukiki kijani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Cuculiformes (Ndege kama kekeo)
Familia: Cuculidae (Ndege walio na mnasaba na kekeo)
Nusufamilia: Phaenicophaeinae (Ndege wanaofanana na malkoha)
Jenasi: Ceuthmocharis (Ukiki)
Cabanis & Heine, 1863
Ngazi za chini

Spishi 2

Ukiki au pundamakaa ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Ceuthmochares katika nusufamilia Phaenicophaeinae ya familia Cuculidae wanaofanana na kekeo. Wana mnasaba na malkoha wa Asia. Wanatokea misitu wa Afrika kusini kwa Sahara. Rangi yao ni buluu au kijani na wana domo njano (kwa sababu ya hii huitwa yellowbill kwa Kiingereza). Hula wadudu wakubwa hasa lakini konokono, vertebrata wadogo, matunda na mbegu pia. Kinyume na kekeo hutengeneza tago lao lenyewe katika mti. Jike hutaga mayai meupe mawili.

Spishi

hariri