Rada (ing. radar) ni jina kwa mitambo inayotumia mawimbi ya redio kutambua vitu na vyombo mbalimbali kwa kuangalia mambo kama aina, mwelekeo, kasi n.k.

Antena ya rada ya masafa maerefu

Rada hutumika kuchunguza ndege, meli, roketi, magari, mawingu katika utabiri wa hali ya hewa, n.k.

Mfumo wa rada unatumia transimita kuzalisha mawimbi ya umeme na sumaku aina ya redio na antena ya kurusha na antena ya kupokea (mara nyingi antena hiyohiyo hutumika kwa kurusha na kupokea) na chombo cha kupokea na kutafsiri kitu kinachochunguzwa.

Rada iliundwa na mataifa kadhaa kwa siri kwa matumizi ya kijeshi katika kipindi cha kabla na wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Viungo vya njeEdit