Rawan Dakik (amezaliwa Arusha, Tanzania, 2 Februari 2001) ni mwanamke Mwafrika wa kwanza na Mtanzania wa pili kupanda kilele cha Mlima Everesti.[1][2]

Rawan Dakik
Amezaliwa 2 Februari 2001
Arusha Tanzania


Rawan Dakik tarehe 22 Mei 2021 alifanikiwa kufika kilele cha mlima Everest ambao ni mlima mrefu kuliko yote duniani ukiwa na urefu wa mita 8,848.

Ameanza kupanda milima mwaka 2012 na tayari ameshapanda milima sita mirefu kwenye mabara tofauti, yaani:

  1. Mlima Kilimanjaro uliopo Kilimanjaro, Tanzania,   barani  Afrika wenye urefu wa mita 5,895.
  2. Mlima Elibras uliopo nchini Urusi,  barani Ulaya una urefu wa mita, 5,648
  3. Mlima Aconcagua uliopo Argentina Barani Amerika ya Kusini una urefu wa mita 6,961.  
  4. Mlima Carstenz Pyramid uliopo nchini Indonesia barani Asia una Urefu wa mita 4,884
  5. Mlima Vinson Massif uliopo Antaktiki wenye urefu wa mita mita 4,892  
  6. Mlima Everest uliopo nchini Nepal barani Asia wenye urefu wa mita 8,848

Kama mazoezi alipanda pia:

  1. Mlima Kazbek wenye urefu wa mita 5,033 uliopo Geogia nchini Urusi
  2. Mwaka 2018 alipanda vilele viwili vya mlima Meru vyenye baridi kali mmoja ukiwa na urefu wa mita 4,562 mlima huo uko Arusha, Tanzania barani Afrika.
  3. Pia alipanda mlima Margherita/Rwanzori uliopo nchini Uganda, barani Afrika.
  4. Milima mingine aliyoipanda ni Mlima Kenya, uliopo nchini Kenya, barani Afrika wenye urefu wa mita 4,985
  5. Mlima Qurnat al Sawda uliopo nchini Lebanon , barani Asia wenye urefu wa mita 3,088
  6. Mlima Faraya uliopo nchini Lebanon barani Asia, wenye urefu wa mita 2,850
  7. Mlima uliopo Sannine nchini Lebanon barani Asia wenye urefu wa mita 2,628
  8. Milima ya Usambara uliopo nchini Tanzania barani Afrika
  9. Mlima Ararat uliopo nchini Uturuki barani Asia wenye urefu wa mita 5,137

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-14. 
  2. https://sautikubwa.org/tanzanian-rawan-dakik-closes-in-on-reaching-mt-everests-peak/

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rawan Dakik kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.