Ray C.
Rehema Chalamila (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Ray C; amezaliwa Iringa, Tanzania, 15 Mei 1982) ni mwimbaji wa muziki wa R&B, dansi, na bongo-bhangra kutoka nchini Tanzania.
Ray C | |
---|---|
Ray C akiwa anatumbuiza
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Rehema Chalamila |
Amezaliwa | 15 Mei 1983 |
Asili yake | Iringa, Tanzania |
Aina ya muziki | R&B, Taarab, dansi, Bongo-bhangra |
Kazi yake | Mwimbaji |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 2002 mpaka leo |
Ame/Wameshirikiana na | Dknob, Chid Benz, Mh Temba, Squeezer, Nako 2 Nako |
Tovuti | MySpace |
Wasifu
haririKabla ya kujihusisha na muziki, Ray C aliwahi kufanya kazi kama mtangazaji wa redio ya East Africa kabla ya kwenda redio ya Clouds FM ya jijini Dar es Salaam.
Mnamo mwaka 2003 alitoa Albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Mapenzi Yangu".
Alianza kujulikana baada ya kutoa vibao kadhaa kama vile, Sikuhitaji, Mapenzi Yangu, Nawewe Milele, Ulinikataa na nyingine nyingi zilizompa umaarufu kama mwimbaji aliyeutingisha muziki wa Bongo Flava kati ya 2003-2009 — hadi hapo alipokuja kuingia matatani kiafya baada ya kutumia dawa za kulevya.
Mwaka wa 2012, Rais wa Tanzania wakati huo, Jakaya Kikwete, alitoa msaada mkubwa wa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ray C na baada ya huduma mwimbaji huyu alikwenda kumshukuru kwa msaada wake.[1]
Mwaka wa 2016 imeripotiwa ya kwamba Ray C amerudi tabia yake ya kutumia dawa za kulevya, hali ambayo ilimkera sana Kikwete.
Muziki
haririAlbamu:
- Mapenzi Yangu (2003)
- Na Wewe Milele (2004)
- Sogea Sogea (2006)
- Touch Me (2008)
Tuzo
haririMshindi:
- 2004 Tanzania Music Awards - Msanii Bora wa kike [2]
- 2004 Kisima Music Awards - Msanii wa kike kutoka Uganda & Tanzania
- 2007 Tanzania Music Awards - Msanii Bora wa kike [3]
Mshiriki:
- 2006 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania)[4]
- 2005 Channel O Music Awards - Msanii bora Afrika ya Mashariki
- 2007 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania)
- 2008 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania) [5]
- 2011 Tanzania Music Awards - Video bora, Wimbo bora, Wimbo bora wa Afro Pop and Wimbo bora wa kushirikishwa ('Mama Ntilie' with Gelly wa Ryme & AT)[6]
Marejeo
hariri- ↑ "Ray C kumtembelea Rais Kikwete Ikulu kwazua hisia tofauti - Bongo5.com", Bongo5.com (kwa American English), 2012-12-11, iliwekwa mnamo 2018-11-17
- ↑ Tanzania Music Awards - Winners 2004
- ↑ Tanzania Music Awards - Winner 2007 Archived 2010-07-10 at the Wayback Machine
- ↑ Musicuganda.com: PAM 2006 nominees Archived 2010-05-22 at the Wayback Machine
- ↑ PAM Awards
- ↑ allAfrica.com: '20 Percent' Grabs Seven Kili Music Awards Nominations
Viungo vya Nje
hariri- Ray C katika Tanzania Directoty.info
- Ray C katika MySpace
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ray C. kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |