Ray Steadman-Allen
Ray Steadman-Allen (18 Septemba 1922 - 15 Desemba 2014) alikuwa mtunzi wa muziki wa Kikristo kutoka Uingereza.
Historia
haririRay alizaliwa katika hospitali ya 'akina Mama' ya Jeshi la Wokovu, mjini Clapton, wakati wazazi wake waliokuwa afisa wa Jeshi la Wokovu walikuwa wakiishi katika eneo la Horfield,Bristol. Walipopata kazi jijini London katika mwaka wa 1937, Ray aliajiriwa kazi katika Makao Makuu ya Kimataifa ya Jeshi la Wokovu kama mtumishi wa ofisi wa Generali Evangeline Booth, binti wa mwanzilishi wa Jeshi la Wokovu.
Katika mwaka wa 1942 aliandikishwa kwenye Kikosi cha Wanamaji. Yeye alitahiniwa kwa shahada ya muziki na Sir Granville Bantock aliyemwalika ili ampe kazi katika muziki vita vitakapoisha. Hapo baadaye, Bantock alikufa, na Ray alijiunga na Idara ya Kuhariri Muziki ya Jeshi la Wokovu. Kufuatia muda mfupi,baada ya vita,alikuwa mchezaji wa ala ya muziki ya tromboni katika Bendi ya Watumishi ya Kimataifa,huko ndiko alikoendeleza ujuzi wake wa kuongoza bendi. Baadaye,alikuwa kiongozi wa Bendi ya Tottenham Citadel.
Akawa afisa wa Jeshi la Wokovu katika mwaka wa 1949, kutoka Harrow corps.
Mnamo mwaka wa 1951,yeye alioa Joyce Foster, ambaye alikuwa afisa Jeshi la Wokovu ya Hastings Citadel tangu 1949.
Kazi katika muziki
haririMuziki wake ilisemekana kama kuwa mbele ya muda yaani ni kama ilikuwa ya wakati ujao hadi wakati mwingine ilikuwa haikubaliki kwa wasikilizaji. Kwa mfano wimbo wake Lord of the Sea ulileta mgogoro mkubwa. Ubunifu wake, kwa kweli, ulikuwa umetoka kwa Mungu na huo ndio ulifanya muziki ya Jeshi la Wokovu kuendelea mbele katika miaka iliyofuata,hasa wakati Idara ya Kimataifa ya Uhariri wa Muziki ilipokuwa chini ya uongozi wake katika miaka ya 1967-1980.
Yeye, mara kwa mara, alishiriki kama Kiongozi wa Bendi katika kipindi maarufu cha Sounding Brass kilichowasilishwa na Gloria Hunniford na Owen Spencer-Thomas katika Radio 2 na Radio London katika miaka ya 1970.
Yeye aliandika kitabu kinachoitwa Colour and Texture in the Brass Band Score ambayo iliyochapishwa na Jeshi la Wokovu. Kilichapishwa kwa mara ya kwanza 1980 na kikakuwa na vichapisho vingi sana baadaye baada ya kutakwa sana na watungaji, waandalizi na idara za muziki za vyuo vikuu.
Mbali na zaidi ya makala ya bendi 200 yaliyochapishwa na Jeshi la Wokovu,aliandika idadi kubwa ya nyimbo,makala ya mabendi na maandalizi katika mpangilio wa kuandika na mkono.
Aidha ya kumaliza Shahada ya juu kabisa katika Muziki, alifanya kazi mbalimbali kama Rais wa Chuo cha Taifa cha Muziki, Naibu wa Rais wa Kikundi cha Viongozi wa Bendi ya Shaba na mdhamini wa Kundi la Utafiti wa Muziki wa London.
Steadman-Allen ,pia, amekuwa mfariji mkubwa wa watu wenye talanta ya kuanzisha aina tofauti ya muziki. Watungaji wengi wa Bendi ya Shaba watapeana ushuhuda juu ya msaada chanya na usaidizi wa kitaalam kutoka kwake.
Katika miaka ya hivi karibuni, Ray Steadman-Allen amekuwa akijulikana kwa jina la utani la 'RSA'.
Katika mwaka wa 2005, Jeshi la Wokovu ilikubali 'RSA' kupewa heshima ya juu kabisa katika Jeshi la Wokovu ambayo mtu anaweza pewa.
Diskografia
hariri- CHRISTMAS CHORAL MUSIC (Danish National Opera Choir)
- BRITISH BANDSMAN CENTENARY CONCERT, 1887-1987
Nyimbo
hariri- Silver Star
- The Eternal Quest
Marejeo
haririViungo vya nje
hariri- Diskografia ya Ray Steadman-Allen Archived 1 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- Vitabu vya Ray Steadman Allen kwenye mtandao Archived 10 Machi 2016 at the Wayback Machine.
- Albamu ya Ray Steadman-Allen