Rebecca Adam

Mwanasheria wa Australia, Mtendaji wa biashara

Rebecca Adam ni wakili wa Australia na mtendaji mkuu wa biashara.[1] Alikuwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo kwa Viziwi (ICSD) kati ya 2018 na 2019, ambapo pia alihudumu kama rais wa zamani wa Michezo ya Viziwi Australia.[2] Mnamo 2018, Agosti, tareahe 1, aliteuliwa kuwa rais wa awamu ya 10 wa ICSD akichukua nafasi ya Valery Rukhledev ambaye alipatikana na hatia ya ubadhirifu kutoka katika Jumuiya ya Viziwi ya All-Russian na alifukuzwa kazi Mei 2018.[3] Aidha, uteuzi wa Rebecca Adam ulizua utata zaidi miongoni mwa mamlaka za michezo ya viziwi ambapo zilitahadharisha kuishtaki ICSD katika Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki.[4][5] Alikuwa mwanamke wa pili pekee, baada ya Donalda Ammons kuchaguliwa kuwa Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Michezo kwa Viziwi.

Utawala

hariri

Rebecca Adam alishikilia wadhifa wa Tume ya Kisheria ya ICSD na kuanzisha Tume ya Michezo ya Wanawake alipokuwa akifanya kazi kama Rais wa Michezo ya Viziwi Australia. Mnamo 2011, baada ya kujiuzulu kama Rais wa Michezo ya Viziwi Australia, aliteuliwa kuwa Bodi ya Wakurungezi ya ICSD.[6]

Rais wa ICSD

hariri

Mnamo 31 Julai 2018, Valery Rukhledev alitangaza kujiuzulu kama Rais wa ICSD kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa dola 803,800 kutoka katika Jumuiya ya Viziwi ya All-Russian ambayo ilimkemea na kukamatwa kwa kuhusika na mashtaka ya kukughushi alipokuwa akihudumu katika wadhifa wa jumuiya hiyo, na wakati akiwa Rais wa ICSD.[7] Aliwekwa kizuizini cha nyumbani kwa zaidi ya miezi miwili na kuishia 23 Julai 2018.[8] Nafasi yake ilichukuliwa na Rebecca Adam mnamo Agosti 1, 2018 baada ya kuchaguliwa kwa kauli moja kushika wadhifa huo hadi 2021, wakati wa mkutano wa kamati ya ICSD.[9] Hata hivyo, tukio hilo lilizua utata zaidi kwani vuguvugu kuu la Wanamichezo Viziwi liliibuka kukosoa uteuzi wa Rebecca Adam wakidai haujafuata taratibu na haujaidhinishwa.[10] Kukamatwa kwa rais wa zamani, Rukhledev kulitia wasiwasi uandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Viziwi ya Majira ya Baridi ya 2019 nchini Italia, lakini baadaye ilithibitishwa kuwa michezo hiyo itaendelea, licha ya kimabadiliko ya kiutawala.[11] Mnamo 13 Septemba 2018, kwenye mkutano wa vyombo vya habari, Rais mteule wa ICSD Rebecca Adam alitoa taarifa akithibitisha kuwa Michezo ya Olimpiki ya Viziwi ya Majira ya Baridi ya 2019 itafanyika kama ilivyokuwa imepangwa na itarabiwa Desemba 2019.[12][13]

Marejeo

hariri
  1. "New chair of the ICSD Women in Sports Commission". www.ciss.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  2. "Presidents". deaflympics.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  3. "President of All-Russian Society of the Deaf arrested for embezzlement". en.crimerussia.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-01. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  4. "Deaf sports crisis deepens after almost 50 countries oppose appointment of new ICSD President". www.insidethegames.biz. Agosti 2018. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "ICSD (Deaflympics) Board Presidential Coup "Unacceptable" AccordingTo ICSD Members". aroundtherings.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-01-01. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  6. "Australia's Rebecca Adam appointed to ICSD Board". www.expression.com.au (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  7. "Press Release: Dr. Valery Rukhledev kept under house arrest for alleged corruption money laundering". www.ciss.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  8. "Deaflympics boss placed under house arrest as part of embezzlement investigation". www.insidethegames.biz. 27 Mei 2018. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Press Release: ICSD Announcement". www.ciss.org (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  10. "Deaf News: Crisis at International Committee of Sports for the Deaf (ICSD)". The Limping Chicken (kwa Kiingereza). 2018-08-03. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  11. "Italy set to host delayed Winter Deaflympics as concerns remain over President arrested in Russia". www.insidethegames.biz. 26 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 2019-01-01.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "ICSD President's Message on 2019 Winter Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  13. "ICSD President's Greeting to the 2019 Winter Deaflympics OC". www.deaflympics.com (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2019-01-01.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rebecca Adam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.