Rema

Muimbaji kutoka nchini Nigeria

Rema (jina halisi ni Divine Ikubor; alizaliwa 1 Mei 2000) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na rapa kutoka Nigeria.

Rema 2024

Alipata umaarufu wa awali kupitia wimbo wake wa 2019 uitwao "Dumebi." Mwaka huo, alisainiwa na lebo ya muziki ya D'Prince[1], Jonzing World. Alipata umaarufu zaidi kupitia wimbo wake wa 2022 uitwao "Calm Down,[2]" wimbo ambao pia aliimba pamoja na mwimbaji wa Mmarekani Selena Gomez na kufikia nafasi ya tatu kwenye chati za Billboard. Wimbo huo pia ulikuwa bora zaidi katika muziki wa Afrobeat kwa wiki 58.

Maisha ya Awali

hariri

Divine Ikubor alizaliwa katika familia ya Kikristo katika Jiji la Benin, Jimbo la Edo, nchini Nigeria. Aligundua mapenzi yake ya muziki wakati wa siku zake za shule ya sekondari katika Kundi la Shule za Ighile katika Jimbo la Edo, ambapo alianza kuimba na kurap. Baada ya kumpoteza baba yake na pia kaka yake mkubwa ambaye alifariki kutokana na masuala ya upasuaji, alilelewa na mama yake pekee. Mnamo tarehe 28 Septemba 2020, Rema alizungumza dhidi ya Peoples Democratic Party (PDP) kwa sababu ya kifo cha baba yake, Jaji Ikubor, kiongozi wa zamani wa chama. Ingawa Rema alipata udahili wa kusoma katika Chuo Kikuu cha Lagos mnamo 2022, alilazimika kuacha chuo hicho mwaka 2023 kwa sababu ya mgomo wa chama cha walimu[3]

Kazi ya Muziki

hariri

2019–2021: Mwanzo wa Kazi Rema alianza kazi yake ya muziki akitumbuiza makanisani na rafiki yake anayeitwa Alpha P. Baada ya kuwa maarufu kwa muziki wake, D'Prince alimsafirisha kwa ndege hadi Lagos na kumpa dili la kurekodi na Jonzing World, lebo ya rekodi ya Nigeria. Mnamo mwaka wa 2019, Rema alitoa albamu yake inayoitwa "Rema" Video ya muziki ya "Dumebi", orodha ya nyimbo kutoka kwa albamu hiyo ilitolewa tarehe ishirini na moja, mwezi wa tano, mwaka wa elfu mbili na kumi na tisa. Baadaye majira ya kiangazi, wimbo mwingine maarufu ulionekana kwenye orodha ya kucheza ya Rais Barack Obama majira ya kiangazi.[4]

2022–23: Rave & Roses na Ravage

hariri

Tarehe ishirini na tano mwezi wa tatu mwaka wa elfu mbili na ishirini na mbili Rema alitoa albamu nyingine inayoitwa "Rave & Roses and Ravage" yenye lebo ya Jonzing World. Albamu hiyo ina nyimbo 16 na ushirikiano na watu kama Chris Brown na zaidi. Wimbo "Calm Down” ulikuwa maarufu wa kimataifa na ulikuwa nambari 3 kwenye Billboard Hot 100 baada ya kufanya kazi na Selena Gomez mwimbaji wa Marekani. Rema alipata tuzo nyingi kwa albamu yake.[5]

2024: HEIS

hariri

Mnamo tarehe kumi na moja mwezi wa saba, mwaka wa elfu mbili na ishirini na nne, Rema alitoa albamu nyingine inayoitwa HEIS. Jina la albamu linatokana na neno la Kigiriki la "nambari 1". Albamu hii ina nyimbo 11 na wasanii maarufu wa Nigeria kama ODUMODUBLVCK kwenye wimbo 'War Machine' na Shallipopi kwenye wimbo 'Benin Boys'[6]

Marejeo

hariri
  1. Nwafor (2019-03-23). "Don Jazzy signs record deal with D'Prince's Jonzing World". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  2. "Rema earns first Billboard Hot 100 entry with 'Calm Down' remix | Pulse Nigeria". www.pulse.ng (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  3. efosataiwo@vanguardngr.com (2023-03-17). "[Video]: I abandoned UNILAG admission because of ASUU strike - Rema". Vanguard News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  4. Charles Holmes (2020-05-15). "How Rema Became Afrobeats' New Superhero". Rolling Stone (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  5. Alphonse Pierre (2019-06-25). "Rema Is Leading the Next Generation of Nigerian Pop". Pitchfork (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  6. Nathan Evans. "Rema: HEIS". Pitchfork (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-12-09.
  Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rema kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.