Reteplasi, yaani Reteplase, yenye majina ya kibiashara kama vile Retavase, ni dawa ya kutibu vidonge vya damu (thrombolytic) ambayo hutumiwa kutibu mshtuko wa moyo.[1] Inaweza pia kutumika kutibu baadhi ya maginjwa ya mishipa ya damu kwenye mapafu kuzibika kwa vidonge vya damu (pulmonary embolisms).[1] Inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kutokwa na damu.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio na ugonjwa na kolesteroli kuziba mishipa ya damu.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Ni aina ya protini inayoungana tena ya kianzishaji plasminojeni ya tishu ya binadamu.[1]

Reteplasi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 1996.[2][4] Nchini Marekani, inagharimu takriban Dola 3,600 kwa kila dozi kufikia 2021.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Reteplase Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Agosti 2019. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "DailyMed - RETAVASE- reteplase kit". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Reteplase Use During Pregnancy". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Rapilysin". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Retavase Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Reteplasi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.