Retifanlimabi, inayouzwa kwa jina la chapa Zynyz, ni dawa inayotumika kutibu Saratani ya Seli za Merkel (Merkel cell carcinoma).[1] Hasa hutumiwa kwa magonjwa ya hali ya juu.[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na uchovu, maumivu ya misuli, kuwashwa, kuhara, homa na kichefuchefu.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya upatanishi wa kinga ya mwili ikiwa ni pamoja na hepatitisi ambayo ni homa ya manjano inayoashiriwa na ini kuvimba, mwasho wa utumbo mpana (colitis), na nimonia na athari za mimenyuko inayotokana na kuingizwa dawa mwilini kwa njia ya mishipa.[1] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[1] Dawa hii ni kingamwili ya monokloni ambayo huzuia kipokezi cha 1 cha kifo kilichopangwa (PD-1).[1]

Retifanlimabi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2023.[1] Nchini Marekani kufikia mwaka wa 2023 dawa hii iligharimu takriban dola 15,000 za Marekani kwa kila dozi.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "DailyMed - ZYNYZ- retifanlimab-dlwr injection". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Zynyz Prices, Coupons, Copay & Patient Assistance". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2023. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Retifanlimabi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.