Revefenasini (Revefenacin), inayouzwa kwa jina la chapa Yupelri, ni dawa inayotumika kwa matibabu ya muda mrefu ya ugonjwa sugu wa mapafu unaozuia (COPD).[1] Inatumika kwa kupumua ndani ya mapafu.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kikohozi, maambukizi ya njia ya juu ya kupumua, maumivu ya kichwa, na maumivu ya mgongo.[2] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio, bronchospasm, na uhifadhi wa mkojo.[1] Ni kipinzani cha muda mrefu cha muscarinic (LAMA).[1]

Revefenasini iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2018.[1] Haijakuwa ikipatikana nchini Uingereza wala Ulaya kufikia 2021.[3] Nchini Marekani inagharimu takriban dola 1,100 za Marekani kwa mwezi.[4]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Revefenacin Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 16 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "DailyMed - YUPELRI- revefenacin solution". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Agosti 2020. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Revefenacin". SPS - Specialist Pharmacy Service. 28 Desemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Oktoba 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Yupelri Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Revefenasini kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.