Rhyme Assassin

Msanii wa Muziki

Rhyme Assassin, (alizaliwa 3 Aprili, 1981), alivyozaliwa alijulikana kama Tichaona Monera, ni mwanamuziki wa hip hop kutoka nchini Zimbabwe anaishi Uingereza, ambaye alianza kung'ara baada ya kuachia kibao chake cha Party People mwaka 2014.[1]

Maisha ya awali

hariri

Rhyme Assassin alizaliwa Chikomba, Chivhu na kukulia mji mkuu wa Zimbabwe katika kitongoji cha Harare na Houghton Park.[2]

Rhyme Assassin alianza muziki mnamo mwaka 2000 akifanya mashindano ya kurap hadi mwaka 2002 alipo ondoka na kuelekea nchini uingereza, akarudia tena maisha yake ya muziki mnamo mwaka 2012, alipokutana na mtayarishaji wa muziki Deep Voice ambaye aliibua tena mapenzi ya Rhyme katika muziki na kuanza kuandika na kurekodi muziki.

Rapa huyu alijizolea umaarufu zaidi mnamo mwaka 2014 baada ya kuachia muziki wake uitwao "Party people" akimshirikisha T9yce. Mziki huu ulikuwa ukishika nambari moja katika vituo vikubwa vya redio huko Zimbabwe na ulikuwa katika chati ya ZBC Power FM ya Zimbabwe kwa muda wa wiki 12 katika vipindi vyote vya kila siku vya Power FM, na pia katika chati ya nyimbo 10, na ya wiki ya nyimbo 20 na kuingia katika 50 bora ya nyimbo 100 kwenye chati ya Power FM ya mwaka 2014[3].[4][5]

Marejeo

hariri
  1. Southern Eye (2013-11-24). "Rhyme Assassin dazzles revellers". Southern Eye (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-06-28. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
  2. "Rhyme Assassin by michelemuscio on DeviantArt". www.deviantart.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-26. Iliwekwa mnamo 2023-02-26.
  4. "Top 10 Zim Hip Hop Songs of 2014". Youth Village Zimbabwe (kwa American English). 2014-12-31. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
  5. "The Urban Radio Hit List - 1 November 2014". Zimbo Jam (kwa American English). 2014-11-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-01. Iliwekwa mnamo 2022-04-26.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rhyme Assassin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.