Rimeksoloni (Rimexolone), inayouzwa kwa jina la chapa Vexol, ni dawa ya steroidi (homoni inayoundwa na binadamu) inayotumika kutibu mwasho wa jicho.[1] Hii ni pamoja na mwasho wa sehemu ya mbele ya jicho (anterior uveitis) na baada ya upasuaji wa jicho.[1] Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuongezeka kwa shinikizo la ndani ya jicho, uoni hafifu, maumivu ya jicho, uwekundu na mafua.[1] Matatizo yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi ya fangasi kwenye konea.[1]

Rimeksoloni iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani katika mwaka wa 1994.[1] Nchini Marekani, chupa ya mililita tano inagharimu takriban dola 100 kufikia mwaka wa 2021.[2] Dawa hii haijakuwa ikipatikana tena nchini Uingereza kufikia mwaka wa 2019.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Rimexolone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 20 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Vexol Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Rimexolone eye drops. Rimexolone antibiotic eye drops - Patient". patient.info (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 17 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rimeksoloni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.