Rodolfo wa Gubbio

Rodolfo wa Gubbio, O.S.B. (Camporeggiano, Umbria, Italia, 1034 - Gubbio, 17 Oktoba 1064) alikuwa mmonaki wa shirika la Wabenedikto na hatimaye askofu wa mji huo kuanzia mwaka 1059.

Mchoro wa Pompeo Batoni ukionyesha Bikira Maria katika kiti cha enzi na Watakatifu na Wenyeheri wa familia Gabrielli wa Gubbio (1736). Venezia, Gallerie dell'Accademia (Rodolfo ni wa kwanza kulia).

Alijitahidi sana kuhubiri na kusaidia maskini bila kuacha kamwe maisha magumu ya toba aliyojifunza kwa Petro Damiani. Hivyo alifariki bado kijana.

Habari zake zinajulikana hasa kutokana na barua ya Petro Damiani, Vita Sancti Rodulphi Episcopi Eugubini.

Tangu kale naheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Juni[1], lakini pia tarehe ya kifo chake.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • San Pier Damiani, Vita Sancti Rodulphi Episcopi Eugubini in: Jacques-Paul Migne, Patrologia Latina, 1844-1855
  • Bernard de Gabrielli, Saint Rodolphe, évêque de Gubbio 1034-1064, 1964
  • Quirico Rughi, Vita di S. Rodolfo Gabrielli vescovo di Gubbio, 1964
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.