Rolapitant, inayouzwa kwa jina la chapa Varubi miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu kichefuchefu na kutapika kunakosababishwa na tiba ya saratani (chemotherapy-induced nausea and vomiting).[1] Inatumika zaidi kwa kichefuchefu ambacho hutokea zaidi ya masaa 24 baada ya tiba ya saratani (chemotherapy).[2] Dawa hii inatumika kwa njia ya mdomo au kwa njia ya sindano kwenye mshipa.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kwikwi (hiccups), kizunguzungu, maumivu ya kichwa na uchovu.[1][2] Dawa hii inaingiliana na mmea wa tiba uitwao St. John's Wort (St. John's Wort)[2] na inafanya kazi kwa kuzuia kipokezi cha NK<sub id="mwIw">1</sub> (kipokezi kinachohusika na shughuli za seli kama vile usafirishaji wa maumivu, utoaji wa homoni na udhibiti wa uzalishwaji wa seli).[2]

Rolapitant iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2015.[3] Iliidhinishwa barani Ulaya mnamo mwaka wa 2017 lakini idhini hiyo iliondolewa baadaye.[4] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 670 za Marekani kwa kila dozi.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 "Rolapitant Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Varuby" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 8 Mei 2020. Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "DailyMed - VARUBI- rolapitant tablet". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Oktoba 2020. Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Varuby". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Juni 2021. Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Varubi Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 18 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rolapitant kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.