Ruhi al-Khalidi (1864–1913) alikuwa mwandishi, mwalimu, mhamasishaji, na mwanasiasa katika Milki ya Osmani mwishoni mwa karne ya kumi na tisa.

Alikuwa mtoto wa ndugu wa Yousef al-Khalidi, ambaye alikuwa meya wa Yerusalemu kuanzia mwaka 1899 hadi 1907.

Mnamo mwaka 1908, alichaguliwa kuwa miongoni mwa wajumbe watatu waliowakilisha Yerusalemu katika serikali mpya ya Osmani iliyoongozwa na vijana wa Kituruki, na baadaye kuwa naibu wa rais wa bunge (1911)

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ruhi Khalidi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.