Ruth Bosibori
Ruth Bosibori Nyangau (pia huandikwa Ruth Bisibori; alizaliwa Bosiango, karibu na Kisii, 2 Januari 1988) ni mwanariadha Mkenya anayekimbia katika mashindano ya umbali wa kati na ni mtaalamu katika shindano la steeplechase mita 3,000.
Mwezi Julai 2007 alikuwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya All-Africa Games, kwani ilishindaniwa mara ya kwanza mwaka huo. Mwezi Agosti mwaka uo huo alimaliza wa nne katika Mashindano ya dunia katika rekodi ya dunia ya wanariadha wachanga ya dakika 9:25.25. Rekodi ya awali ilikuwa 9:30.70 ilikuwa imewekwa na Melissa Rollison. [1]. Alimaliza wa tatu katika mashindano ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2008.
Bosibori alianza kukimbia mwaka 2003 alipokuwa katika chuo cha upili cha Kebirichi. Aliajiriwa na Polisi wa Kenya baada ya kushinda michuano ya mkoa mwaka 2007. Amezoea kukimbia miguu mitupu.[2]
Alishinda tuzo la Mwanariadha wa kike ambaye ana ahadi zaidi mwaka 2007 katika sherehe za Kenya Sports Personality of the Year[3] Kocha wake ni Dan Muchoki [4]
Mafanikio
haririmwaka | Mchuano | Ukumbi | Tokeo | Ziada |
---|---|---|---|---|
2007 | All-Africa Games | Alger, Algeria | 1 | 3000 m steeple |
World Championships | Osaka, Japan | 4 | 3000 m steeple | |
2008 | African Championships | Addis Ababa, Ethiopia | 3 | 3000 m steeple |
Michezo ya Olimpiki | Beijing, Uchina | 6 | 3000 m steeple | |
World Athletics Final | Stuttgart, Ujerumani | 3 | 3000 m steeple | |
2009 | World Championships | Berlin, Ujerumani | 7 | 3000 m steeple |
World Athletics Final | Thessaloniki, Grekland | 1 | 3000 m s'chase |
Tanbihi
hariri- ↑ IAAF top orodha - 3000 mita Steeplechase Junior
- ↑ Japan Times, 29 Agosti 2007: Worlds notebook; Day 4
- ↑ "Soya Awards - 2007 winners". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-13. Iliwekwa mnamo 2009-12-18.
- ↑ IAAF: 4 Agosti 2007: Focus on Africa - Ruta BOSIBORI Ilihifadhiwa 2 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
hariri- IAAF wasifu wa Ruth Bosibori
- Pace Sports Management Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ruth Bosibori kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |