Sturmabteilung

(Elekezwa kutoka SA)

Sturmabteilung (Kikosi cha mashambulizi - kifupi cha Kijerumani SA) ilikuwa kitengo cha wanamgambo wa chama cha NSDAP cha Adolf Hitler katika Ujerumani kuanzia 1921 hadi 1945.

Askari wa SA wadogo wa kuwachezea watoto
Kikosi cha SA chasimama nyuma ya Adolf Hitler
Bendera ya SA

Chanzo kama walinzi wa mikutano

hariri

Ilianzishwa 1921 kama kikosi cha kulinda mikutano ya NSDAP iliyovurugwa mara nyingi na wapinzani waliosikitika matamshi ya Hitler. Hitler aliweza kutumia wanajeshi walioachishwa jeshini baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kiongozi wa SA alikuwa kapteni Ernst Röhm.

Sare za kahawia

hariri

SA ilivaa sare za rangi ya kahawia zilizopatikana kwa bei nafuu kwa sababu zilikuwa mabaki ya vita. Kikosi kilipiga marufuku pamoja na chama cha NSDAP mwaka 1923 na kuundwa upya 1925. Wakati ule kikosi maalumu kilundwa ndani ya SA kwa ajili ya ulinzi wa Hitler mwenyewe. Kikosi hiki cha Schutzstaffel (SS) kilitengwa baadaye na SA kama mkono wa pekee wa chama cha Nazi. SS ilivaa sare nyeusi.

Kazi ya SA ilikuwa maandamano wakivaa sare zao na kuonyesha kuwepo kwa chama barabarani. Ilitumiwa pia kuvuruga mikutano na maandamano ya vyama vingine na kulinda mikutano ya chama.

Jeshi la Chama

hariri

Tangu matatizo ya kiuchumi ya kimataifa ya 1929 Wajerumani wengi walikuwa bila ajira. Katika hali hii idadi ya wanaSA ikaongezeka sana. Mwaka 1930 ilikuwa na wanamgambo 60,000 waliongezeka kuwa 220,000 hadi 1932 na 400,000 hadi 1934.

Katika kempeni ya uchaguzi wa bunge wa 1932 watu 300 waliuawa katika mapigano kati ya SA na wanamgambo Wa vyama vingine.

Baada ya Hitler kushika serikali alitumia vikosi vya SA kutisha wapinzani wake. WanaSA walikamata wapinzani hovyo na kuwapiga. Bunge la 1933 lililokuwa na wapinzani mwanzoni lilipaswa kukutana ilhali wanamgambo wa SA walijaza ukumbi wa mkutano.

Hitler amaliza uongozi wa SA na upinzani ndani ya chama

hariri

WanaSA wengi walitegemea mapinduzi ya kumalizia ubepari kwa sababu waliamnini matangazo ya Hitler aliposhambulia mabepari. Lakini Hitler hakuwa na nia hiyo hivyo sehemu za SA walianza kulalamika kati yao.

Mwaka 1934 Hitler aliamua kuwaondoa viongozi wa SA. Katika usiku moja viongozi wakubwa walikamatwa na wanaSS. Takriban watu 130 waliuawa. Viongozi wa NSDAP walitumia nafasi ya kuuawa pia wapinzani wengine katika usiku uleule. Baadaye walitangaza ya kwamba Viongozi hawa wa SA walipanga mapinduzi lakini walizuiliwa.

Kwa tendo hiki Hitler alimaliza dhana zote za upinzani ndani ya chama chake ya NSDAP dhidi yeye menyewe.

SA baada ya 1934

hariri

SA iliendelea kama kitengo kikubwa cha NSDAP chini ya viongozi wapya lakini umuhimu wake ulipungua sana. Walipewa tena kazi mwaka 1938 katika mashambulio dhidi ya Wayahudi katika Ujerumani walipochoma moto masinagogi katika Ujerumani na kuvunja nyumba za Wayahudi.