Shirika la Riadha la Kenya

(Elekezwa kutoka SRK)

Shirika la Riadha la Kenya linalojulikana kama AK ni jumuia linazosimamia Riadha nchini Kenya. Shirika hili ni memba wa IAAF na Shirikisho la Riadha Afrika. AK huratibu mashindano ya Riadha nchini Kenya. Pia hutuma timu ya Kenya kushiriki katika mashindano ya kimataifa. Isaiah Kiplagat ndiye mwenyekiti sasa hivi wa Riahda nchini Kenya. AK ina ofisi zake kuu katika Riadha House, karibu na Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo, Nairobi.

Historia

hariri

Shirika hili lilikuwa likijulikana kama Shirikisho la Amecha Kenya mpaka mwaka wa 2002. Shirikisho ilianzishwa katika ukoloni Kenya mwaka wa 1952 na marehemu Derek Erskine.

Kenya ni taifa lenye ustadi katika Riadha, lakini talanta hii huishia katika mbio za mbali. Wanariadha maarufu wa Kenya kwa kawaida hutoka wilaya kama Keiyo, Marakwet na Nandi katika magharibi ya Kenya. Karibu wote huwa kabila la Kalenjin.

Mashindano makuu ya kwanza ya kimataifa ambako Kenya ilishiriki ilikuwa michezo ya Ulaya ya 1954, huko Cardiff, lakini Kenya haikushinda medali yoyote.

Mashindano ya Kenya hufanyika katika misimu ya joto, lakini majaribio tofauti hutumika kubaini wanariadha kwa michuano ya kimataifa. Wanariadha mabingwa wa Kenya kwa kawaida huhudhuria matukio hayo, manake wale wanaozikosa huenda kuwa wanakosa michuano mikubwa vilevile. Wanariadha wengi wa Kenya hushindana Ulaya, michuano ya kitaifa na majaribu ni tukio tu ambapo watazamaji wanaweza kuwatazama wakishindana.

Mashindano mengine yanayoandaliwa na Shirika la Riadha la Kenya ni kama mfululizo wa mbio za nyika na zingine za barabarani. Kenya husimamia matukio ya mbio mara tatu kila mwaka. Mbio za nyika za Nairobi ilianza majuzi, lakini sasa inaongoza katika ushindani na ushiriki. Zingine ni Mbio za nyika za Mombasa na ile ya Ziwa Kuu, inayofanyika mjini Kisumu. Isitoshe, kuna ushindani unaojulikana kama , ambayo inahusisha mashindano mawili sawa na (42 km) na nusu Mbio za nyika, lakini ni mbio ya nyika kwa hivyo haiwezi linganishwa na Mbio za nyika. Hata hivyo, tukio la Mbio za nyika za Lewa limewavutia wakenya wakimbiani wengi wa kimataifa na limeshindwa na Paul Tergat, Catherine Ndereba na Joyce Chepchumba katika miaka iliyopita.

Wakimbiaji wengi wakenya hujihusisha na mashirika ya kiserikali kama vile Jeshi la Kenya, shirika la magereza Kenya au Polisi wa Kenya, ambayo huwapa riziki pamoja na mazoezi. Aidha, kuna vilabu binafsi kadhaa vya riadha, kama vile Mfae (mjini Nyahururu) na Kiptenden (inayopatikana Kericho).

Shirika la Riadha la Kenya hufanya kazi kama makumbusho katika Nyumba ya Riadha, Nairobi. Makumbusho hayo yalifunguliwa tarehe 1 Novemba 2006 [0]

Shirika la Riadha la Kenya ilipatiwa tuzo mwaka 2006 kwa kuwa Shirikisho bora Kenya mwakani [1]

Wenyeviti

hariri

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri