Sade
Helen Folasade Adu (amezaliwa 16 Januari 1959) ni mwanamuziki kutoka nchi ya Nigeria. Anajulikana zaidi kwa jina la Sade. Sade ambaye amewahi kupata Tuzo ya Grammy hasa ni mwimbaji na mtunzi.
Sade | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Helen Folasade Adu |
Amezaliwa | 16 Januari 1959 Ibadan, Jimbo la Oyo, Nigeria |
Asili yake | London, Uingereza |
Aina ya muziki | Soul, jazz, R&B, quiet storm, soft rock, adult contemporary |
Kazi yake | Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi |
Aina ya sauti | contralto |
Miaka ya kazi | 1980–mpaka sasa |
Studio | Portrait/CBS Records Epic/SME Records |
Ame/Wameshirikiana na | Sade |
Tovuti | www.sade.com |
Historia
haririSade alizaliwa katika mji wa Ibadan katika Jimbo la Oyo. Baba yake, Bisi Adu, alikuwa ni Mnigeria, mhadhiri wa masuala ya uchumi, na mama yake, Anne Hayes, alikuwa ni nesi toka Uingereza. Baada ya baba na mama yake kuachana, mama yake alirudi Uingereza ambapo aliwachukua Sade na kaka yake, Banji. Akiwa Uingereza, Sade alijenga mapenzi na masuala ya mitindo, dansi, na kuimba. Wakati huo alipenda kuwasikiliza wanamuziki kama Marvin Gaye, Curtis Mayfield, na Donny Hathaway.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sade kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |