Samli
Samli (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: clarified butter au ghee) ni mafuta yanayotokana na malai yanayoelea juu ya maziwa ya wanyama kama vile ng'ombe, ngamia au mbuzi na ambayo yanatumiwa kupikia nyama, mboga n.k.
Kimsingi ni malai ambayo maji ndani yake yameondolewa au angalau kupunguzwa kwa kiasi kikubwa. Samli inayotokea hudumu muda mrefu kuliko malai au siagi hata bila jokofu kwenye halijoto ya wastani.
Mara nyingi samli hutengenezwa kwa kupasha joto siagi hadi maji yameondoka. Inawezekana pia kuipata moja kwa moja kutoka malai yanayokusanywa na kupashwa moto.
Katika tiba
haririPia ni mafuta yanayotumika sana kama tiba asilia ya nguvu za kiume kwa wanaume, hasa yanapotumika pamoja na asali mbichi na kitunguu maji au yakichanganywa na mafuta ya nyonyo na kisha kuchua uume.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Samli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |