Semaglutidi
Semaglutidi (Semaglutide), inayouzwa kwa majina ya chapa ya Ozempic miongoni mwa mengineyo, ni dawa inayotumika kutibu Kisukari aina ya 2 na unene uliokithiri.[1] Haipendekezwi sana kuliko metformin, ingawa zote mbili zinaweza kutumika pamoja.[1][2] Dawa hii inaboresha udhibiti wa sukari ya damu, hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo, na kupunguza hatari ya matatizo ya figo.[1] Inatumika kwa kupitia mdomoni au kwa kudungwa sindano chini ya ngozi.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo, na kuvimbiwa choo.[1] Madhara yake makubwa yanaweza kujumuisha ugonjwa wa kisukari wa asidi nyingi damuni, sukari ya chini ya damu, na kongosho.[2] Kuna wasiwasi kwamba matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto, na kutumia wakati wa kunyonyesha hakupendekezwi.[1] Dawa hii inafanya kazi kama glukagoni ya kibinadamu iliyo kama peptidi-1 (GLP-1) na huongeza kutolewa kwa insulini, inapunguza kutolewa kwa glukagoni, na kupunguza uondoaji wa votu tumboni.[2]
Semaglutidi iliidhinishwa kwa matumizi ya matibabu nchini Marekani katika mwaka wa 2017.[1] Iliundwa na shirika la Novo Nordisk[1] na ilikuwa GLP-1 ya kwanza ambayo inaweza kuchukuliwa kupitia njia ya mdomo. Nchini Uingereza, miligramu mbili za sindano iligharimu Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) takriban £73 kufikia mwaka wa 2020.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kiligharimu takriban Dola 850 kufikia mwaka wa 2021. [3]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Semaglutide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 2 Aprili 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 738. ISBN 978-0-85711-369-6.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link) - ↑ "Ozempic Prices, Coupons & Savings Tips". GoodRx (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 16 Aprili 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)