Sesili wa Karthago

Sesili wa Karthago (jina lake kamili kwa Kilatini lilikuwa Caecilianus[1]) alikuwa padri wa mji huo (katika eneo la Tunisia ya leo) katika karne ya 3.

Mtu mwadilifu, ni maarufu hasa kwa kumsaidia Sipriani kuongokea Ukristo (245).

Kabla hajafa, Sesili alimkabidhi Sipriani kazi ya kutunza mke na watoto wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Juni[2][3].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. Taz. "Vita Sancti Cypriani" kilichoandikwa na shemasi Ponsyo; Jeromu kimakosa alimuita Caecilius tu (De viris illustribus, 67, PL, XXIII, 714), na jina hilo fupi limezoeleka
  2. Martyrologium Romanum
  3. https://catholicsaints.info/saint-caecilius-of-carthage/
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.