Sevelameri (Sevelamer), inayouzwa kwa jina la chapa Renagel miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu hyperphosphatemia katika ugonjwa sugu wa figo.[1] Nchini Uingereza ni matibabu ya mstari wa pili.[2] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo pamoja na milo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuhara, kichefuchefu, na kuvimbiwa.[1] Upele wa ngozi unaweza pia kutokea.[2] Inafanya kazi kwa kuifunga fosfati kwenye matumbo.[1]

Sevelameri iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1998.[1] Nchini Marekani inagharimu takribani dola 48 za Marekani kwa vidonge 270 vya miligramu 800 kufikia mwaka wa 2021.[3] Kiasi hiki nchini Uingereza kinagharimu Huduma za Afya za Kitaifa (NHS) takriban £75.[2]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Sevelamer Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Novemba 2020. Iliwekwa mnamo 12 Oktoba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 BNF (tol. la 80). BMJ Group and the Pharmaceutical Press. Septemba 2020 – Machi 2021. uk. 1116. ISBN 978-0-85711-369-6.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: date format (link)
  3. "Sevelamer Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 7 Aprili 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sevelameri kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.