Severino Kiwango ni mwongozaji wa filamu za kiTanzania. Ikiwa ni Mpenzi wa kuangalia vipindi vya Luninga lazima uta mfahamu huyu Bwana Severino kiwango amewahi kuongoza michezo mingi sana katika Televisheni ya ITV hasa ile ya kizamani wakina Mzee Jongo, michezo ya kaole hapo mwanzoni kabisa na sasa hivi yupo kwenye masuala ya Filamu za Kitanzania ndiko anako shughulika moja kati ya Filamu alizo ongoza ni 'Misukosuko' 1 na 2. Kiwango pia ni Mtayarishaji wa kwanza wa vipindi vya Televisheni ya rangi barani Africa. Kiwango pia ameshiriki kwenye vita vya Tanzania na Uganda kama Mwongozaji (Director) wa Filamu ya mapambano vitani. Vilevile Kiwango aliongoza vipindi vya mahakamani vya kesi ya rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume. Pia aliongoza upigaji picha wa tukio la kuunganishwa kwa vyama vya TANU na AFRO-SHIRAZ. Kiwango ndiye pia aliyeongoza upigaji picha wa maziko ya Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere. Huyu ndiye mtanzania wa kwanza kusomea mambo ya Televisheni na Filamu, Hollywood nchini Marekani. Katika medani za siasa, Kiwango alikuwa mmoja wa walioanzisha Chipukizi wa Afro-Shiraz na CCM. Kwa sasa Kiwango ni Mtayarishaji Mkuu (Chief Producer) wa vipindi vya ITV (IPP) na pia ni Mkufunzi (Visiting) wa mambo ya Televisheni katika chuo Kikuu cha Tumaini, Iringa.


Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Severino Kiwango kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.